Watu 21 wauwawa katika ajali ya mgodi wa makaa ya mawe | Habari za Ulimwengu | DW | 07.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Watu 21 wauwawa katika ajali ya mgodi wa makaa ya mawe

-

BEIJING

Watu 21 wamefariki katika ajali iliyotokea kwenye mgodi wa makaa ya mawe kaskazini mwa China.Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari vya serikali chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana ingawa wachimba mawe hao walikwama chini ya mgodi tangu jumamosi asubuhi.

Watu 11 wamefanikiwa kunusurika ajali na wameshaokolewa.Migodi ya makaa ya mawe nchini China ni miongoni mwa migodi hatari kabisa duniani ambapo viwango vya usalama vinapuuzwa mara kwa mara na kusababisha ajali.Mwaka jana pekee kiasi watu 3,800 walikufa katika migodi hiyo ya makaa ya mawe nchini humo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com