Watoto watano wakutikana wamekufa Ujerumani | Habari za Ulimwengu | DW | 06.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Watoto watano wakutikana wamekufa Ujerumani

BERLIN

Watoto watano wenye umri kati ya miaka mitatu na tisa wamekutikana wakiwa wamekufa kwenye nyumba moja katika kijiji cha Darry kaskazini mwa Ujerumani hapo jana.

Mama wa watoto hao mwenye umri wa miaka 34 anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika na maua ji ya watoto hao na amewekwa katika hospitali ya magonjwa ya akili.

Polisi imesema bado inaendelea na uchunguzi na imekataa kutowa maelezo zaidi .

Mama wa watoto hao amejisalimisha mwenyewe kwa polisi na radio moja ya Ujerumani imesema watoto hao wote ni wavulana na kwamba mama huyo aliwalewesha kabla ya kuwauwa kwa kuwaziba pumzi kwa kutumia mifuko ya plastiki.

Darry ni mji wenye wakaazi 450 na uko kilomita 40 mashariki mwa Kiel karibu na Bahari ya Baltik nchini Ujerumani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com