WASHINGTON.Bush kuwasilisha bajeti ya vita vya Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 05.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON.Bush kuwasilisha bajeti ya vita vya Irak

Rais George Bush wa Marekani anapanga kuwasilisha bajeti ya vita vya Irak itakayo fikia takriban dola bilioni mia tatu kwa kipindi cha miaka miwili na nusu ijayo.

Bush anatarajiwa kupendekeza upungufu katika matumizi ya ndani katika mwaka 2008.

Bajeti hiyo ambayo pia inahusisha asilimia 10.5 ya ongezeko katika bajeti ya kijeshi ni ya kwanza kufikishwa mbele ya Kongress inayothibitiwa na chama cha Demokratik.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com