WASHINGTON:Bush atangaza vikwazo zaidi dhidi ya Myanmar | Habari za Ulimwengu | DW | 20.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON:Bush atangaza vikwazo zaidi dhidi ya Myanmar

WASHINGTON

Rais Gorge W Bush wa Marekani ametangaza vikwazo vikali zaidi dhidi ya utawala wa kijeshi wa Myanmar.

Rais Bush amesema kufuatia mauaji na utesaji unaofanywa na utawala huo wa kijeshi anataka vikwazo zaidi kwa viongozi wa nchi hiyo..

Aidha Katika taarifa iliyotolewa na ikulu ya White House rais Bush ameamrisha kwamba vikwazo vya sasa vya kibiashara dhidi ya nchi hiyo viongezwe.Ametaka vikwazo vya usafiri viwakabili viongozi zaidi katika utawala huo na kufungwa kwa akaunti zao.

Ameusisitizia utawala huo wa kijeshi usiotaka Demokrasia uwaachie huru wafungwa wakisiasa na kuingia katika meza ya mazungumzo na chama cha Upinzani kinachotetea demokrasia.Hatua ya rais Bush imekuja siku kadhaa baada ya Umoja wa ualya kutangaza kwamba inaongeza vikwazo dhidi ya utawala huo wa kijeshi wa Myanmar.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com