WASHINGTON: Majeshi ya Marekani kupata kiongozi mpya | Habari za Ulimwengu | DW | 09.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Majeshi ya Marekani kupata kiongozi mpya

Admirali wa vikosi vya wanamaji wa Marekani,Mike Mullen anatazamiwa kuwa kiongozi mpya wa majeshi ya Marekani.Waziri wa ulinzi wa Marekani,Robert Gates amemteua Mullen kuchukua nafasi ya Peter Pace atakaemaliza kipindi chake cha miaka miwili.Alipozungumza mjini Washington,waziri Gates alisema,Jemadari Peter Pace ataondoka madarakani mwisho wa mwezi Septemba.Gates ametaka Jemadari Pace aendelee kwa awamu ya pili,lakini vyama vyote viwili katika bunge la Marekani vinampinga Pace,anaejulikana kwa msimamo wake wa kuunga mkono kuwepo kwa Marekani nchini Irak.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com