Wajerumani wengi waiona serikali ya muungano imegawika
14 Agosti 2025
Utafiti huo umeonesha kwamba asilimia 32 tu ya walioulizwa wanaamini kuwa vyama vilivyo kwenye serikali hiyo ya muungano vinashirikiana vyema, huku asilimia 61 wakiamini kuwa hakuna ushirikiano kati ya vyama hivyo, wakiwemo asilimia 41 ya wafuasi wa chama cha Kihafidhina cha Christioan Democratic Union na asilimia 47 ya wafuasi wa chama cha Kisoshalisti cha SPD.
Mwanzoni mwa mwezi mei, siku chache kabla serikalihiyo kuingia mamlakani, ni asilimia 51 ya watu tu walioamini kwamba vyama hivyo vitashirikiana vyema katika majukumu ya kuiongoza serikali.
Utafiti huo uliwahusisha watu 1,370 walio na haki ya kupiga kura na ulifanywa kwa njia ya simu na mtandao kati ya Agosti 11 na 13 mwaka 2025.
Kulingana na utafiti huo, iwapo uchaguzi wa shirikisho utafanywa sasa basi serikali hiyo ya muungano haitopata wingi unaohitajika kuunda serikali.
Serikali ya muungano ya Ujerumani inajumuisha vyama ndugu vya Kihafidhina CDU/CSU na chama cha Kisoshalisti cha SPD.