Waislamu nchini Kenya Waandamana dhidi ya kukamatwa kwa Mhubiri wa Kijamaica | Matukio ya Kisiasa | DW | 15.01.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Waislamu nchini Kenya Waandamana dhidi ya kukamatwa kwa Mhubiri wa Kijamaica

Nchini Kenya Waislamu leo hii wameandamana dhidi ya kukamatwa kwa Mhubiri wa Jamaica Sheikh Abdullah Al Faisal.

default

Jiji la Nairobi kulikofanyika maandamano kupinga kukamatwa kwa sheikh Al Faisal

Mzozo kuhusu kukamatwa kwa mhubiri raia wa kutoka Jamaica, Sheikh Abdulla Al Faisal, umechukuwa sura mpya baada ya jamii ya Waislamu nchini humo kuandamana leo kuishinikiza serikali kumuachilia huru mara moja Mhubiri huyo, anayetuhumiwa kuwa mfuasi wa kundi la kigaidi la Al Qaeda.

Katika mji mkuu wa Nairobi, Polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatimua wandamanaji hao na watu watano wadaiwa kufa.

Katika mji wa Mombasa kama anavyoarifu mwandishi wetu Eric Ponda pia kulifanyika maandamano hayo.

Mwandishi:Eric Ponda

Mhariri:Aboubakary Liongo

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com