Vikosi vya usalama vya Libya vapatiwa mafunzo na polisi wa Ujerumani | Habari za Ulimwengu | DW | 06.04.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Vikosi vya usalama vya Libya vapatiwa mafunzo na polisi wa Ujerumani

Berlin:

Kisa cha kupatiwa mafunzo vikosi vya usalama vya Libya na askari polisi wa Ujerumani kinagonga vichwa vya habari na kuwashughulisha wanasiasa wa humu nchini.Habari za ahivi karibuni zinasema kisa hicho huenda kinafungamana na kuachiwa huru famailia Wallert mnamo mwaka 2000.Gazeti la Bild am Sonntag, sawa na gazeti la BERLINER ZEITUNG yakinukuu duru za idara za upelelezi yameripoti katika toleo la leo kwamba Libya iliyosaidia katika kuwachiwa huru familia Wallert,ilishauri badala yake vikosi vyake vya usalama vipatiwe mafunzo na polisi wa Ujerumani.Kansela wa zamani Gerhard Schröder na kiongozi wa Libya Muammar Kaddafi waliokutana miaka minne baadae kwa ziara rasmi,wakatia saini mkataba wa ushirikiano.Familia Wallert na watalii wengine 18 walitekwa nyara jumapili ya pasaka mwaka 2000 na wafuasi wa itikadi kali ya dini ya kiislam na kushikiliwa miezi kadhaa nchini Philippine.Inasemekana Libya ililipa dala milioni 21wakati ule ili mahabusi hao waachiliwe huru.

 • Tarehe 06.04.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Dcss
 • Tarehe 06.04.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Dcss
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com