Vijana wa Ujerumani chini ya miaka 21 mabingwa wa Ulaya. | Michezo | DW | 30.06.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Vijana wa Ujerumani chini ya miaka 21 mabingwa wa Ulaya.

Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 21 mabingwa wapya bara la Ulaya.

default

Mabingwa wa bara la Ulaya chini ya miaka 21- Ujerumani wakishangilia bao lao la kwanza lililowekwa wavuni na Gonzalo Castro .

Timu ya taifa ya Ujerumani ya vijana wa umri chini ya miaka 21, kwa mara ya kwanza kabisa imefanikiwa kunyakua taji la ubingwa wa bara la Ulaya, kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya vijana kutoka Uingereza katika fainali jana usiku.

Mabao mawili yaliyowekwa wavuni na mshambuliaji kutoka club ya Duisburg Sandro Wagner yalikamilisha ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Uingereza kwa Ujerumani katika fainali ya ubingwa kwa vijana chini ya miaka 21 na kuwapa ushindi wao wa kwanza katika historia ya mashindano hayo.

Wajerumani , ambao wameongeza taji hili juu ya mataji mengine baada ya vijana , chini ya miaka 17 na 19 kunyakua ubingwa wa makundi yao, pia walipata mabao yao ya kwanza kupitia Gonzalo Castro pamoja na Mesut Özil.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Uingereza kufika katika fainali tangu mwaka 1984 na pia kufikisha mwisho wa kutoshindwa katika mlolongo wa michezo 21 na kutoa kumbukumbu kwa kocha wa Ujerumani Hosrt Hrubesch ya mafanikio aliyoyapata wakati akiwa kama mchezaji katika timu ya taifa ya wakati huo ya Ujerumani magharibi katika mwaka 1980 katika fainali ya kombe la bara la Ulaya.

Tumeweza kuonyesha uwezo wetu katika mashindano haya. Michezo yetu mitatu ya kwanza ukiondoa ule wa Hispania haikuwa mizuri. Nusu fainali ilipoanza hali ilianza kuwa nzuri na hivi sasa tunaweza kusema, vijana wameonyesha kile wanachokiweza.


Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Stuart Pearce amesema kuwa ataendelea kuifunza timu ya vijana chini ya miaka 21 kwa ajili ya mashindano yajayo ya 2011 na kujaribu kuinua kiwango kutoka hiki cha sasa.

Uingereza ilianza vizuri mchezo huo huku Adam Johnson alichonga korosi kadha za hatari wakati James Milner , akiwa anacheza kwa mara yake ya 49 katika timu hiyo na ambayo ni mara ya mwisho kwa vijana wa chini ya umri wa miaka 21, alichonga mkwaju maridadi wa free kick na Martin Cranie alipiga kichwa nje.

Baada ya Ujerumani kufunga bao la kuongoza, walikuta wakicheza kwa kuelewana zaidi na kwa kujiamini. Baada ya hapo walikuwa wakijaribu kila mara kusukuma mipira mbele na kutengeneza nafasi nyingi za kupata mabao.

Tulikuwa tumejitayarisha vya kutosha kwa mchezo huu, kila mmoja alikuwa akimsaidia mwingine. Na wakati huo huo tuliweza kusukuma mbele mashambulizi, kitu ambacho ilikuwa vigumu kutoshinda. Na sasa tunafurahia ushindi.


Kwa ushindi huu vijana wa Ujerumani wamelipiza kisasi kwani katika fainali ya mwaka 1982 Uingereza ilishinda kwa mabao 2-1. Kwa chama cha kandanda cha Ujerumani Deutsche Fusball bund , DFB, ushindi huu kwa kiasi fulani ni maalum, kwa kuwa hakuna timu ya vijana chini ya umri wa miaka 21 ya Ujerumani iliyowahi kushinda kombe hili, hii ni mara ya kwanza. Hivi sasa Ujerumani inashikilia ubingwa wa vikombe vitatu vya bara la Ulaya, chini ya miaka 17, chini ya miaka 19 na 21.

►◄
 • Tarehe 30.06.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Ie1v
 • Tarehe 30.06.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Ie1v
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com