1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yalaani mashambulizi ya anga ya Israel nchini Syria

Sylvia Mwehozi
30 Machi 2024

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi Maria Zakharova, amesema kuwa vitendo hivyo vya kichokozi dhidi ya Syria ni ukiukaji wa wazi wa mamlaka ya nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4eGtq
Damascus | Syria
Uharibifu wa mashambulizi ya Israel mjini Damascus januari 2024Picha: Ammar Ghali/Anadolu/picture alliance

Urusi imelaani mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Israel nchini Syria, ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 40. Wapiganaji 9 na kamanda wauwawa kwa mashambulizi SyriaMsemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi Maria Zakharova, amesema kuwa vitendo hivyo vya kichokozi dhidi ya Syria ni ukiukaji wa wazi wa mamlaka ya nchi hiyo na kanuni za kimsingi za sheria ya kimataifa na hayakubaliki kabisa.

Zakharova ameongeza kuwa Urusi inalaani vitendo hivyo ambavyo vina athari kubwa ya kuchochea zaidi mzozo wa Palestina na Israel.

Shirika linalofuatilia haki za binadamu la Syria lenye makao yake makuu Uingereza, lilisema siku ya Ijumaa kwamba mashambulizi ya anga ya Israel iliyoyafanya upande wa Kaskazini mwa Syria, yaliwaua askari 36 na wapiganaji wanne wa kundi la Hezbollah. Urusi ni mshirika muhimu wa rais wa Syria Bashar Al Assad.