1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi 36 wauwawa katika shambulizi la Israel, Aleppo

Amina Mjahid
29 Machi 2024

Shirika la uangalizi wa haki za binaadamu la Syria SOHR, limesema wanajeshi 36 wa Syria wameuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulizi la angani lililofanywa na Israel Kaskazini mwa mji wa Aleppo.

https://p.dw.com/p/4eFaJ
Syria, shambulizi la Aleppo
Picha za Setilaiti zinazouonyesha mji ulioshambuliwa wa AleppoPicha: Planet Labs PBC/AP/picture alliance

Shirika hilo ambalo limekuwa likifuatilia vurugu zinazoendelea Syria tangu mwaka 2011, limesema mashambulizi hayo yaliyotokea alfajiri ya leo yalilenga bohari la silaha linalomilikiwa na wanamgambo wa Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran.  

Wanajeshi wa Israel washambulia eneo la makaazi ya watu katika mji wa Damascus Syria

Mashambulizi hayo yaliyotokea katika eneo la Jibreen karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Aleppo pia yalisababisha mauaji ya wanamgambo sita wa Hezbollah.

Kiongozi wa shirika hilo la SOHR Rami Abdel Rahman, amesema idadi ya waliouwawa huenda ikapanda kufuatia watu kujeruhiwa vibaya katika shambulio hilo. Hata hivyo jeshi la Israel halijatoa tamko lolote hadi sasa kufuatia madai hayo.