1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel yashambulia eneo la makaazi ya watu mjini Damascus

Saumu Mwasimba
21 Februari 2024

Wanajeshi wa Israel wameshambulia kwenye mji mkuu wa Syria Damascus,na kulenga eneo la makaazi ya watu.

https://p.dw.com/p/4cgna
Matingatinga yakiondoa vifusi katika jengo lililoharibiwa baada ya shambulio la Israel mjini Damascus
Matingatinga yakiondoa vifusi katika jengo lililoharibiwa baada ya shambulio la Israel mjini DamascusPicha: Ammar Ghali/Anadolu/picture alliance

Ripoti hizo zimetangazwa leo Jumatano na shirika la habari la SANA linaloendeshwa na serikali ya Syria.

Shirika hilo bila ya kutowa ufafanuzi zaidi limesema mashambulizi ya Israel yamelenga eneo la makaazi la Kafr Sousa huku wakaazi wa eneo hilo wakiliambia shirika la habari la kijerumani DPA kwamba walisikia sauti za miripuko na kuona moto ukiwaka kwenye baadhi ya nyumba za watu katika jengo moja lililoko karibu na shule.

Shirika linalofuatilia hali ya haki za binadamu nchini Syria lenye makao yake Uingereza limesema hii ni mara ya 13 Israel kuishambulia Syria mwaka huu.