1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yatoa wito wa mchango wa kukabiliana na nzige Afrika

Amina Mjahid
11 Februari 2020

Mjumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulika na masuala ya kiutu ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuzisaidia nchi za Afrika Mashariki zilizoathirika na uvamizi wa makundi ya nzige wa jangwani.

https://p.dw.com/p/3XaZO
Wüstenheuschrecken werden auf einem Weideland im Dorf Nakwamuru
Picha: Reuters/N. Mwangi

Mark Lowcock amekiambia kikao cha wanahabari kuwa kuna watu milioni 13 katika nchi zilizoathirika ambao wanakabiliwa na kitisho kikubwa cha uhaba wa chakula sasa.

Watu milioni kumi kati yao wapo katika maeneo yaliyoathirika na nzige hao.

Lowcock ambaye amesema hivi karibuni alitoa kiasi cha dola milioni 10 kupambana na janga hilo, alionya kuwa kama hapatakuwa na suluhisho la haraka, kutakuwa na tatizo kubwa baadaye mwaka huu.

Nzige hao wameharibu vyakula nchini Kenya, Ethiopia na Somalia. Wameripotiwa kuvamia Uganda Jumapili.