1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU imeituhumu Urusi kwa uhalifu wa kivita Ukraine

Sudi Mnette
25 Machi 2022

Umoja wa Ulaya umeituhumu Urusi kwa Uhalifu wa kivita nchini Ukraine. Kwa mujibu wa azimio la viongozi wa umoja huo Urusi itaadhibiwa kwa sheria za kimatiafa.

https://p.dw.com/p/490vY
Die Staats- und Regierungschefs der Europäischen Union treffen sich inmitten der russischen Invasion in der Ukraine in Brüssel
Picha: Olivier Matthys/AP/picture alliance

Umoja huo umesema baada ya mkutano wao wa kilele wa mjini Brusseles, serikali ya Urusi itawajibishwa kwa mujibu wa sheria za kimataifa.  Azimio la Baraza la Umoja wa Ulaya linasema Urusi imekuwa ikiratibu mashambulizi dhidi ya umma wa watu na kuyalenga maeneo ya umma, vikiwemo hospitali, viwanda vya madawa, shule na makazi. Na kumalizia huo ni uhalifu wa kivita lazima usitishwe mara moja.

Mataifa yenye nguvu ya kiviwanda yaionya Urusi dhidi ya matumizi ya silaha za kemikali.

Die Staats- und Regierungschefs der Europäischen Union treffen sich inmitten der russischen Invasion in der Ukraine in Brüssel
Rais Joe Biden na viongozi wa UlayaPicha: Adam Schultz/White House/IMAGO

Na kundi la mataifa yenye nguvu ya kiwanda duniani yaani G7 yameonya dhidi ya kutumika kwa silaha yoyote ya maangamizi dhidi ya Ukraine, kwa kusema Urusi inadhibitiwa na mikataba ya kimataifa.

Baada ya mkutano wao wa kilele wa dharura kuhusu uvamizi wa Ukraine, taarifa ya pamoja ya mataifa hayo ilitoa onyo la kutumika kwa silaha za kikemikali, bailojoia, nyuklia au zozote zenye kufanana na hizo. Imeitaka Urusi kutimiza matakwa ya makubaliano ya kimataifa,ambayo Urusi imesaini ya kulinda kila mmoja.

Rais Joe Biden kufanya ziara katika eneo la mpaka wa Poland na Ukraine.

Katika taarifa yake ya sasa Ikulu ya Marekani imesema Rais Joe Biden leo hii atatembelea mji wa Poland ambao uko karibu na mpaka na Ukraine, kwa lengo la kuonesha mshikamano na Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Katika eneo hilo la Rzesow, lililo umbali wa kilometa 50 kutoka mpakani mwa Ukraine, Biden atakutana na Rais wa Poland, Andrzej Duda. Ni sehemu ya safari yake ya dharura barani Ulaya ambayo imesababisha na vita vya Ukraine.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken amesema katika ziara yake ya Machi 5 alilitembelea eneo hilo kwa lengo la kuonesha uungaji wake mkono kwa wanajeshi wa NATO, kwa iliyokuwa seheumu ya Jumuiya ya Kisovieti.

Ikulu ya Marekani inasema katika ziara hiyo ya Ijumaa hii pia, Biden atapokea taarifa ya namna gani Poland inakabiliana na wimbi la mamilioni ya wakimbizi ambao wanakimbia makombora ya Urusi huko Ukraine. Aidha atakutana na wanajeshi wa kikosi cha anga ambao wana kambi yao katika eneo hilo la Rzeszw.

Vita vya Ukraine na wasiwasi wa China katika mahusano yake na Urusi.

Katika hatua nyingine afisa wa ngazi ya juu ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani Colin Kahl amesema vita vya Ukraine vimeibibisha China jukumu zito katika mahusiano yake na Urusi. Amesemna anadahani kuna kiwango cha mambo kinachofanywa na Urusi nchini Ukraine ambacho kimefanya jambo hilo kuwa gumu kwa China, kuliko ilivyokuwa wiki sita iliyopita au miezi sita.

Mwezi Februari, China na Urusi zilitangaza uhusano usio na kikomo, katika kuungana mkono katika mizozo ya Ukraine na Taiwan, na kushirikiana zaidi dhidi ya matiafa ya Magharibi.

Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri amepigiwa simu na mwenziwe wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ambapöo katika mazungumzo yao Sisi amesisitiza umuhimua wa mazungumzo na suluhu ya kidemokrasia katika utatuzi wa vita vinavyoendelea. Taarifa hiyo ni kwea mujibu wa ofisi ya rais wa Misri.

Wabunge wa Ukraine jana Alhamisi wamepiga kura kumwadhibi yeyote anaisaidia Urusi akiwa ndani ya taifa hulo kuhukumiwa kifungo hadi cha miaka 12 gerezani. Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya bunge la taifa hilo vitendo hivyo ni pamoja na kuunga mkono, kusafirisha fedha na usaidizi wowote kwa jershi la Urusi.

Pamoja na adhabu ya kifungo, mtu atakaekutwa na hatia pia atazuiwa kufanya kazi serikalini katika kipindi cha miaka 15 na mali zake kutaifishwa.

Vyanzo: RTR/AFP