Biashara
EU na Indonesia kutia saini makubaliano ya kibiashara
22 Septemba 2025
Matangazo
Makubaliano hayo, yatakayotiwa saini katika kisiwa cha mapumziko cha Bali, yataiunganisha Indonesia yenye rasilimali na jumuiya ya Ulaya yenye wanachama 27 katika uhusiano wa karibu wa kiuchumi.
Hayo yanakuwa ni makubaliano ya tatu ya kibiashara kati ya Umoja wa Ulaya umetia na nchi za kusini mashariki mwa Asia, baada ya Singapore na Vietnam.
Umoja wa Ulaya ni mshirika mkubwa wa tano wa kibiashara wa Indonesia na biashara ya pande hizi mbili ilifikia dola bilioni 30.1 mwaka jana.