Umoja wa Ulaya mbioni kuuidhinisha mfuko wa kuokoa uchumi | Matukio ya Kisiasa | DW | 14.07.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Umoja wa Ulaya

Umoja wa Ulaya mbioni kuuidhinisha mfuko wa kuokoa uchumi

Mataifa ya Umoja wa Ulaya hayajafikia makubaliano ya pamoja juu ya mpango ya mfuko wa kusaidia uchumi wa nchi za jumuia hiyo kutokana na janga la corona.

Viongozi wa mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya wanajiandaa kukutana siku ya Ijumaa kwa mara ya kwanza tangu mwezi Februari kwa ajili ya kufanikisha makubaliano juu ya mfuko wa euro bilioni 500 za kusaidia uchumi wa nchi za Umoja wa Ulaya. Kiasi hicho cha fedha kilichopendekezwa na Ujerumani na Ufaransa.

Mfuko huo ni wa kuzisaidia nchi zilioathirika zaidi kiuchumi na janga la virusi vya corona. Italia na Uhispania zikiwemo kwenye orodha hiyo. Baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya zinaupinga mpango huo wa Ufaransa na Ujerumani.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel (Reuters/K. Nietfeld)

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel mnamo siku ya Jumatatu alimpokea Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte kwa mazungumzo katika nyumba ya wageni ya serikali ya Meseberg kaskazini mwa mji mkuu, Berlin.

Mazungumzo kati ya viongozi hao wawili yalilenga masuala ya uchumi na athari za kijamii zilizosababishwa na janga la corona, ambapo Italia ni nchi mojawapo iliyoathirika vibaya sana.

Mjadala huo umeongezwa katika majadiliano ya bajeti ya nchi 27 wanachama wa jumuiya ya Umoja wa Ulaya ambazo pia zimo kwenye mjadala kuhusu Brexit. Leo Jumanne jioni kansela Merkel atakutana na Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez katika juhudi za kupata uungwaji mkono wa mfuko wa kuzisaidia nchi za Umoja wa Ulaya zilizoathirika zaidi na janga la corona.

Halmashauri Kuu Angela Merkeya Umoja wa Ulaya imependekeza kiasi cha euro bilioni 750 kwa ajili ya mpango huo kabambe wa kuuokoa uchumi wa umoja huo unaojumuisha euro bilioni 500 zitakazotolewa kama misaada na euro bilioni 250 kwa ajili ya mikopo.

Vyanzo:AP/DPA

 

 

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com