1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumbe wa Urusi wakutana na wajumbe wa Trump Florida

12 Machi 2026

Ujumbe wa Urusi ukiongozwa na mjumbe maalum wa Rais Vladimir Putin, Kirill Dmitriev, umekutana na ujumbe wa Marekani huko Florida siku ya Jumatano.

https://p.dw.com/p/5AD8W
Moscow 2025 | Mjumbe maalum wa Rais Vladimir Putin, Kirill Dmitriev
Mjumbe Maalum wa Rais wa Urusi kuhusu Uwekezaji wa Kigeni na Ushirikiano wa Kiuchumi KirillPicha: Sergei Bulkin/ZUMAPRESS/picture alliance

Ujumbe wa Urusi ukiongozwa na mjumbe maalum wa Rais Vladimir Putin, Kirill Dmitriev, umekutana na ujumbe wa Marekani huko Florida siku ya Jumatano, ikiwa ni mara yao ya kwanza tangu kuanza kwa vita kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Kulingana na mjumbe maalum wa Marekani Steve Witkoff, timu hizo zilijadili masuala mbalimbali na zimekubaliana kuendelea kuwasiliana.

Mazungumzo hayo yanakuja baada ya Marekani mapema wiki hii kuondoa baadhi ya vikwazo dhidi ya mafuta ya Urusi, vilivyowekwa kutokana na uvamizi wa Moscow nchini Ukraine mwaka 2022 ili kupunguza bei za mafuta katikati mwa vita na Iran.

Trump alisema wiki hii kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin, ambaye alizungumza naye Jumatatu, anataka kusaidia kuhusiana na vita vya Mashariki ya Kati.