1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumbe wa Iran wavamiwa na kukamatwa na jeshi la Marekani

Saumu Mwasimba29 Agosti 2007

Ubalozi wa Iran nchini Iraq umesema wanajeshi wa Marekani wamewakata wajumbe wake saba waliokuwa kwenye ujumbe wa wizara yake ya Nishati waliokwenda mjini Baghdad.

https://p.dw.com/p/CH8u
Picha: AP

Shirika la habari la Iran limesema ujumbe huo wa Iran uliopaswa kutia saini makubaliano ya Nishati na wenzao wa Iraq ulikamatwa baada ya jeshi la Marekani kuivamia Hoteli ya Sheraton walikokuwa. Wajumbe hao wa Iran waliwekwa ndani ya magari na kupelekwa mahala pasipo julikana.Tukio hili limekuja muda mfupi baada ya rais Goerge Bush kusema katika Hotuba yake huko Nevada

‘’Iran haiwezi kuepuka dhamana ya kuhusika katika mashambulio dhidi ya majeshi ya muungano pamoja na kuwauwa raia wa Iraq wasio na hatia,Iran lazima ikomeshe vitendo vyake na hadi itakapofanya hivyo nitachukua hatua zinazostahili kuwalinda wanajeshi wetu na nimeamrisha makamanda wa jeshi letu nchini Iraq kukabiliana na shughuli za mauaji zinazofanywa na Tehran.’’

Aidha rais Bush amesema ikiwa Iran itaruhusiwa kujipatia silaha za kinuklia italiweka hatarini eneo zima la mashariki ya kati.

Awali rais wa Iran Mahmoud AhmedNejad alionya kwamba ushawishi wa serikali ya Marekani katika eneo hilo unasambaratika kwa haraka na Iran itakuwa tayari kuchukua nafasi hiyo.