1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yasema amani haiwezekani Mashariki ya Kati

Grace Kabogo
8 Desemba 2023

Serikali ya Ujerumani imesema amani ya kudumu katika Mashariki ya Kati haiwezekani, iwapo kundi la Hamas litaendeleza mashambulizi kutoka Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4ZwrO
Gaza Konflikt zwischen Israel und der palästinensischen islamistischen Gruppe Hamas
Hali baada ya mashambulizi ya Israel kwenye eneo la Khan Younis kusini mwa Ukanda wa Gaza siku ya Ijumaa (Disemba 8).Picha: AFP

Akizungumza na waandishi habari mjini Berlin, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani amesema leo kuwa kwa sasa wanahimiza usitishwaji zaidi wa mapigano.

Wizara hiyo imesema kuwa Israel inapaswa kuzuia raia kuteseka katika eneo la kusini la Ukanda wa Gaza, na inawajibika kutii sheria za kibinaadamu.

Soma zaidi: Wizara ya Afya wa Gaza, imesema Wapalestina wapatao 17,177 wameuawa na wengine 46,000 kujeruhiwa katika mashambulizi yaliyoanza Oktoba 7.

Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ameitaka Israel kuongeza juhudi za kuwalinda raia huko Gaza.

Aidha, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linakutana leo kujadili vita vya Gaza.

Umoja wa Falme za Kiarabu uliwasilisha rasimu mpya ya azimio kutaka kusitishwa kwa mapigano huko Gaza.