1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yapinga kupunguza gesi zinazotolewa na magari

20 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CdwB

BERLIN

Serikali ya Ujerumani imeelezea kukasirishwa kwake juu ya mpango wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya wa kuanzisha sheria kali ya kupunguza utowaji wa gesi za carbon dio oxide kutoka kwenye magari.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema mpango huo utaipa mzigo mkubwa usio na kifani Ujerumani na kampuni zake za kutengeneza magari.Waziri wa Mazingira wa Ujerumani Sigmar Gabriel ameuita mpango huo kuwa vita vya ushindani dhidi ya vivanda vya magari nchini Ujerumani ambavyo vitawanufaisha washindani wao wa Ufaransa na Italia ambao hutengeneza magari mepesi kwa kulinganishwa na yale ya Ujerumani.

Wakati wa mkutano mjini Brussels Ubelgiji chombo hicho kikuu tendaji cha Umoja wa Ulaya kilipendekeza kupunguzwa kwa kima cha gesi ya carbon dioxide kwa magari ya abiria kutoka gramu 160 hadi kuwa gramu 120 ifikapo mwaka 2012.

Pendekezo hilo sasa linabidi liidhinishwe na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.