1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaionya Urusi dhidi ya shambulizi la mtandao

Lilian Mtono
3 Mei 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ameionya Urusi kwamba itakabiliwa na hatua kali baada ya kuzishutumu idara zake za kijasusi za kijeshi kwa kupanga shambulizi la hali ya juu kabisa la mtandaoni.

https://p.dw.com/p/4fTCL
Annalena Baerbock akiwa Australia
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena BaerbockPicha: Sina Schuldt/dpa/picture alliance

Baerbock amewashutumu wadukuzi wa serikali ya Urusi kwa kupanga shambulizi la mtandaoni mwaka uliopita lililokilenga chama cha kisiasa cha Social Democrat, SPD, kinachoongoza serikali ya mseto nchini Ujerumani.

Amesema hilo halivumiliki na halikubaliki na kutakuwa na majibu. 

Watu 13 wajeruhiwa Odessa kufuatia shambulio la Urusi

Uhusiano kati ya nchi hizo mbili za Ulaya tayari uko mashakani na hasa kutokana na hatua ya Ujerumani ya kuisaidia kijeshi Ukraine katika vita yake dhidi ya Urusi.