Ujerumani yainusuru Benki ya Mikopo ya Nyumba
6 Oktoba 2008Matangazo
Makubaliano hayo mapya ya kiasi cha euro billioni 50 ya kuipatia benki hiyo ambayo ni ya pili kwa ukubwa hapa Ujerumani, yalifuatia kushindwa mpango wa awali wa euro billioni 35 zilizokuwa zitolewe na taasisi nyingine za fedha.
Mapema Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alitangaza mipango ya kuhakikisha usalama wa fedha za watu binafsi katika mabenki kufuatia mzozo huo wa kibenki.
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa pamoja na Waziri wa Fedha wa Ujerumani Peer Steinbrueck, mjini Berlin Kansela Merkel aliahidi kudhibiti msukosuko huo katika mfumo wa fedha na kuongeza kuwa ana daiwa na walipa kodi wa Ujerumani kuchukua hatua hatua mujaribu.