Ujerumani yailaumu Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 12.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ujerumani yailaumu Marekani

BALI.Waziri wa Mazingira wa Ujerumani Sigmar Gabriel ameilaumu Marekani kwa msimamo inaouchukua katika suala la mabadiliko ya hali ya hewa.

Akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa huko Bali Indonesia, Sigmar amesema kuwa Marekani imekuwa kikwazo katika harakati za kimataifa kufikia mkataba mpya wa hali ya hewa.

Mapema Katibu Mkuu wa Mataifa Ban Ki moon alitoa wito kwa nchi zote kukubaliana na mkataba wa kupambana na ongezeko la ujoto duniani ifikapo mwaka 2009.

Mawaziri wa Mazingira na wakuu kadhaa wa serikali watatumia siku tatu za mwisho za mkutano huo kujaribu kuweka muundo wa kupambana na mabadiliko ya hali hewa kabla ya mwaka 2012 wakati mkataba wa Kyoto utakapomalizika.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com