Imetimia miaka 36 tangu kuangushwa ukuta wa Berlin
9 Novemba 2025
Matangazo
Rais Frank-Walter Steinmeier atakuwa mwenyeji wa hafla ya kukumbuka siku hiyo pamoja na ghasia za mwaka 1938 dhidi ya Wayahudi. Steinmeier anatazamiwa pia kutoa hotuba katika makazi yake mjini Berlin itakayojikita katika kuimarisha demokrasia.
Kumbukumbu ya maumivu na chuki dhidi ya Wayahudi
Ofisi yake imesema kuwa Novemba 9 inaakisi kuibuka kwa mwangaza wa uhuru na demokrasia, pamoja na kumbukumbu ya maumivu na chuki dhidi ya Wayahudi.
Ukuta wa Berlin uliangushwa Novemba 9 mwaka 1989 na siku hiyo inaadhimishwa Ujerumani kama mwisho wa udikteta wa iliyokuwa Ujerumani Mashariki na kushindwa na itikadi ya kikomunisti ya Dola ya Kisovieti.