Ujerumani na Uingereza Wembley | Michezo | DW | 23.08.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Ujerumani na Uingereza Wembley

Mbele ya viongozi wa nchi hizo mbili-waziri mkuu G.Brown na Kanzela Angela Merkel, Ujerumani na Uingereza ziliondoka uwanjani 2:1.Ujerumani kwahivyo, ikalipiza kisasi cha aibu ya Munich, 2001.

Per Mertesacker, kulia, na Christoph Metzelder, kushoto, wa timu ya Ujerumani

Per Mertesacker, kulia, na Christoph Metzelder, kushoto, wa timu ya Ujerumani

Ujerumani ililipiza kisasi chake jana kwa kuizaba Uingereza mabao 2:1 na kufuta aibu ya mjini Munich,2001 ilipokandikwa mabao 5:1 na Uingereza.Ujerumani ikiwa timu ya mwisho kuilaza England katika uwanja wa zamani wa Wembley, ilikuwa pia ya kwanza jana kuilaza Uingereza katika uwanja wake mpya wa Wembly. Waziri-mkuu wa Uingereza na kanzela wa Ujerumani Angela Merkel, walikuwapo binafsi uwanjani Wembley.

Ingawa matokeo ya jana hayakuonesha kuwa Uingereza ilikua hafifu mbele ya wajerumani,matokeo ya jana yameonesha Uingereza imeshinda hadi sasa mechi 2 tu kati ya 9 iliocheza chini ya kocha wao mpya-nazo dhidi ya chipukizi Estonia na Andorra.Hii haitoi matumaini kwa kinyanganyiro cha mwezi ujao cha kuania tiketi za kombe la ulaya 2008 nchini Uswisi.

Alikuwa mchezaji wa kiungo wa Chelsea Frank Lampard alielifumania kwanza lango la ujerumani mnamo dakika ya 9 ya mchezo.Madhambi yaliofanywa na kipa wa Uingereza Paul Robinson yaliadhibiwa na mshambulizi wa Schalke,Kevin Kuranyi aliesawazisha mnamo dakika ya 26 ya mchezo.

Halafu akiichezea kwa mara ya kwanza Ujerumani,mlinzi wa shoto wa Schalke Christian Pander,aliutandika mkwaju maridadi ajabu mnamo dakika ya 40 ya mchezo na kubadili mkondo wa mchezo usiku wa jana.

Wajerumani wakalipiza kisasi chao kwa England iliowazaba mabao 5:1 mjini Munich.Ujerumani ikaishinda Uingereza kwa bao 1:0 hapo oktoba 2000 katika uwanja wa zamani wa Wembley.

Kocha wa Uingereza Steve McClaren ,baada ya mechi ya jana alieleza hivi jinsi mchezo ulivyokwenda:

„Dakika 20 za kwanza nadhani tilitamba zaidi na tukiongoza mchezo,lakini baadaye tukapunguza kasi na kuwaachia wajerumani kucheza.Ikabidi hapo kucheza kwa ujasiri na tulipata fursa za kutia bao,lakini hatukujaaliwa kuwa usiku wetu siki hiyo.“

Kocha wa Ujerumani,Joachim Loew alisema mbinu yake ya kumzuwia David Beckham kutojipatia nafasi ya kupiga mikwaju ya freekick karibu na lango la Jens Lehmann-kipa wa Ujerumani, ndio ufunguo wa ushindi wa jana wa mabao 2:1 uwanjani Wembley.

Holland ikirudi kucheza na ruud van Niestelrooy,ilizabwa pia mabao 2:1 na Uswisi,mwenyeji wa kombe lijalo la Ulaya.

Brazil ilitokwa na jasho kabla kuizima Algeria mjini Montpellier,Ufaransa kwa mabao 2:0.Beki wa Brazil Maicon ndie alieufumania kwanza mlango wa Algeria baada ya kupita saa nzima.

Ronaldinho ambae pamoja na kaka hawakuchezeshwa tangu mwanzo,ndie alieipatia Brazil bao la pili.

Ronaldinho atazamiwa kupatiwa uraia wapili wa Spain,jumatatu ijayo.

Mabingwa wa dunia Itali,walikiona kilichomtoa kanga manyoya mbele ya Hungary.Wamezabwa mabao 3:1.

Akijinoa kwa changamoto zinazoanza keshokutwa jumamosi za ubingwa wa riadha ulimwenguni huko Osaka, japan,muethiopia Kenenisa Bekele bingwa wa mita 5000 na 10.000 amefichua leo kwamba alikumbana na simba wakati wa mazowezi yake nyumbani kwa mashindano haya ya Osaka.

Alisema alimuona simba karibu na kambi yake ya mazowezi katika kitongoji cha Addis Ababa.Yeye na nduguye,wakamuachia simba huyo na mwanawe wapite kabla kufyatuka upya mbio.

 • Tarehe 23.08.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHbC
 • Tarehe 23.08.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHbC