Ujerumani na Austria zatishiwa kushambuliwa | Habari za Ulimwengu | DW | 21.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ujerumani na Austria zatishiwa kushambuliwa

Ukanda mpya wa video wa watuhumiwa wanamgambo wa itikadi kali za Kiislam umetolewa kwenye mtandao ukitishia kufanya mashambulizi dhidi ya Ujerumani na Austria iwapo nchi hizo hazioondowa wanajeshi wao kutoka Afghanistan .

Ukanda huo umeonyeshwa na televisheni ya Austria hapo jana jioni.Wanamgambo hao wamejitambulisha kuwa the Global Islamist Media Front.

Ujerumani ina wanajeshi 3,000 waliowekwa nchini Afghanistan ikiwa ni sehemu ya kikosi cha Kimataifa cha Usaidizi wa Usalama ISAF kinachoongozwa na Jumuiya ya Kujihami ya Mataifa ya Magharibi NATO.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Wolfgang Schäuble amesema serikali inaungalia ukanda huo kwa makini lakini Ujerumani haigopeshwi na vitisho

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com