Uchumi wa Ujerumani unatazamiwa kukua mwaka huu | Matukio ya Kisiasa | DW | 15.04.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Uchumi wa Ujerumani unatazamiwa kukua mwaka huu

Uchumi wa Ujerumani unatazamiwa kukua kwa asilimia 1.5 katika mwaka huu wa 2010 wakati soko la ajira likibakia imara. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na taasisi maarufu za utafiti wa uchumi nchini Ujerumani.

Die Vertreter führender Wirtschaftsforschungsinstitute, Joachim Scheide (Kiel), Volker Nitsch (Zürich), Axel Lindner (Halle), Roland Döhrn (Essen) und Kai Carstensen (München, l-r) stehen am Donnerstag (23.04.2009) während einer Pressekonferenz in Berlin nebeneinander. Die Forscher stellten das Frühjahrsgutachten bzw. die Prognose für die Wirtschaft der Jahre 2009 und 2010 vor. Die Arbeiten waren vom Ministerium für Wirtschaft und Technologie in Auftrag gegeben worden. Foto: Soeren Stache dpa +++(c) dpa - Report+++

Wajumbe wa taasisi kuu tano za utafiti wa uchumi duniani.

Ripoti iliyotolewa leo hii mjini Berlin na taasisi tano maarufu zinazofanya utafiti wa uchumi duniani, inasema, uchumi wa Ujerumani uliodorora wakati wa majira ya baridi, sasa umeanza kufufuka.Inatathminiwa kuwa katika mwaka huu wa 2010, pato la jumla la ndani nchini Ujerumani litaongezeka kwa asilimia moja na nusu. Lakini mwakani uchumi huo unatazamiwa kukua kwa asilimia moja nukta nne.

Wataalamu wa uchumi wanasema mauzo ya nje yaliyoimarika ndio yaliosaidia kwa sehemu kubwa . Hata matumizi ya wateja yaliyoongezeka yamechangia kufufua uchumi wa Ujerumani. Wakati huo huo, idadi ya wasio na ajira inatazamiwa kupunguka pole pole, lakini sio kwa sababu ya kuongezeka nafasi za ajira, bali watu wanahamia kule kunakopatikana kazi.

Wataalamu hao wanasema,hali ya uchumi hivi sasa inatia moyo, lakini kile kiwango cha kabla ya msukosuko wa fedha kutokea,hakitazamiwi kufikiwa kabla ya mwaka 2013. Na masoko ya fedha bado ni tatizo kubwa kwani hakuna maendeleo ya maana yaliyopatikana katika sekta hiyo.Vile vile mradi wa serikali unaosaidia sekta ya uchumi unamalizika mwakani na hiyo ni barabara, wanasema wataalamu hao wa uchumi. Kwa maoni yao, mwakani, serikali ianze kupunguza madeni yake. Inatathminiwa kuwa nakisi ya bajeti ya serikali katika mwaka huu itafikia asilimia 4.9 ya pato la jumla la ndani na mwakani asilimia 4.2. Lakini kwa mujibu wa mpango ulioidhinishwa na Umoja wa Ulaya katika jitahada za kupata utulivu na ukuaji wa uchumi, nakisi ya bajeti isivuke asilimia 3 ya pato la ndani.

Kinachotia wasiwasi ni kuwa sio tu gharama za kuimarisha uchumi zilizoongezeka bali matumizi ya serikali pia yameongezeka sana. Ripoti hiyo inaikosoa serikali ya Ujerumani kuwa bado haijaeleza vipi inapanga kushughulikia bajeti yake. Joachim Scheide alie mkuu wa kitengo cha utafiti katika taasisi ya uchumi iliyoko mjini Kiel Ujerumani anawakosoa wanasiasa kuwa wanachojadili wakati wote huu ni suala la kupunguza malipo ya kodi ya mapato na sio deni la taifa. Yeye anasema, mradi njia ya kupunguza pengo litakalosababishwa na hatua ya kupunguzwa kodi ya mapato, bado haijulikani, basi itakuwa bora kuliachilia mbali suala hilo.

Mwandishi:Martin,Prema/AFPD

Mhariri:Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com