Rais wa sasa Paul Kagame anatarajiwa kuwashinda wapinazni watatu waliomuunga mkono katika uchaguzi wa mwaka 2003
Rais wa Rwanda, Paul Kagame, akipiga kura katika shule ya Echo Ruganga katikati mwa Kigali leo
Wanyarwanda hii leo wanapiga kura kumchagua rais mpya katika uchaguzi wa pili wa rais tangu kumalizika mauaji ya halaiki ya mwaka 1994. Rais wa sasa wa Rwanda, Paul Kagame, ambaye anatarajiwa kushinda awamu nyengine ya miaka saba, amepuuzilia mbali madai ya ukandamizaji wa wapinzani na kusisitiza kuwa uchaguzi wa leo wa rais umefanyika kwa njia ya kidemokrasia. Peter Moss amezungumza hivi na mwandishi wetu wa Rwanda, Daniel Gakuba.