Uchaguzi wa Kenya - Rais Mwai Kibaki atangaza timu ya kampeni
27 Septemba 2007Matangazo
Kiongozi wa taifa anapanga kuzindua rasmi kampeni ya chama cha PNU jumapili hii. Timu hiyo ilitangazwa na kundi la Kibaki tena linalosimamia kampeni za Rais kibaki kuteuliwa tena. Timu hiyo maalum inaongozwa na Rais Kibaki mwenyewe na makamu wa rais Moody Awori akiwa msaidizi wake.
Thelma Mwadzaya amezungumza na Profesa Tom Namwamba mhadhiri wa filosofia katika Chuo Kikuu cha Kenyatta kuhusu tukio hilo.