Uchaguzi nchini Guinea kufanyika Disemba mwaka huu. | Matukio ya Kisiasa | DW | 05.05.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Uchaguzi nchini Guinea kufanyika Disemba mwaka huu.

Kapteni Moussa Dadis Camara, aliyakua madaraka katika mapinduzi ya kijeshi kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Lasana Conte aliyefariki mwezi Disemba mwaka jana.

Kapteni Moussa Dadis Camara.

Kapteni Moussa Dadis Camara.

Uthabiti wa kisiasa nchini Guinea umo mikononi mwa utawala wa kijeshi, ambao umeahidi kufanyika kwa uchaguzi wa rais hivi karibuni.Kapteni Moussa Dadis Camara aliyenyakua madaraka katika mapinduzi ya kijeshi alijaza nafasi iliyoachwa wazi na rais Lasana Conte aliyefariki dunia mwezi December mwaka jana , baada ya kutawala kwa karibu miaka 25.

Mapinduzi yasiyokuwa ya umwagikaji damu na majeshi nchini Guinea yalileta afueni kwa baadhi ya wachunguzi ambao walihofia kutokea kwa machafuko baada ya kifo cha rais Conte.Hivi sasa wanasiasa wa upinzani ,vyama vya wafanyakazi na hata baadhi ya mabalozi wa kigeni wameoneka kuridhika na utawala huo wa kijeshi.


Camara kutoka chama cha National Council and Democracy and development-CNDD, amepata uungaji mkono kutokana na ajenda yake maarufu ya kukabiliana na ufisadi katika taifa hilo maskini, kukabiliana na ulanguzi wa madawa ya kulevya na kuangalia upya mikataba na makampuni ya kigeni ya madini,mengi yanaonekana kuwapunja waGuinea.


"Tunakiunga mkono chama cha CNDD hadi kufanyika kwa uchaguzi anasema Jean Marie Dore, aliyekuwa mgombea urais na kiongozi wa chama maarufu cha upinzani cha Union for progress of Guinea-UPG. Iwapo wataamua kubakia madarakani kufuati uamuzi wa upande mmoja huenda kukatokea matatizo, lakini iwapo ni kwa kupitia makubaliano kila kitu kitakuwa shwari".


Camara ameapa kuandaa uchaguzi mwezi December na makundi ya kisiasa na kijamii yamebaini kuwa kwa kukipinga chama cha CNDD juhudi zao kupata demokrasia zitatizikwa hata zaidi. "Vyama vya kisiasa na mashirika ya kijamii yameamua kukiunga mkono chama cha CNDD kwasababu iwapo kutatokea hali ya kutoelewana itachangia kuwepo kwa kipindi kirefu kabla ya mabadiliko ya utawala.


Vyama vya wafanyakazi vinakiunga mkono chama cha CNDD kwa hivi sasa, japokuwa baada ya mzozo kati ya wafanyakazi na kampuni moja yachuma kutoka Urusi ,Camara aliegemea upande wa kampuni hiyo.


Makampuni ya madini ambayo huiletea Guinea pato la kigeni na kutoa ajira kwa maelfu ya waguinea yameelezea wasiwasi wao kuhusiana na njisi Camara anavyojiingiza lakini wiki iliyopita waziri wa madini aliahidi kuwepo kwa hali ya maelewano.


Makampuni ya kigeni pia yangependa kufanyika kwa uchaguzi.Rio Tintos mkurugenzi mkuu wa kampuni moja nchini humo amesema serikali iliyochaguliwa kwa njia ya demokrasia itawahakikishia wawekezaji kuwa Guinea ni eneo salama kutumia fedha zao.


Mashirika ya kimataifa yamekosoa kuchukua madaraka kwa bw Camara.Umoja wa Afrika na jumuiya ya ushirikano wa kiuchumi wa nchi za afrika magharibi-ECOWAS tayari zimesimamisha uwanachama wa Guinea hatua inayochukuliwa dhidi ya taifa lolote kutoka bara Afrika ambako kuna hali ya madaraka kunyakuliwa kwa nguvu. Nyengine ni Mauritania na hivi karibuni Madagascar.


Lakini katika mkutano na wawakilishi wa utawala wa kijeshi na umoja wa ulaya mjini Brussels nchini Ubelgiji wiki iliyopita,kamishna wa maendeleo wa umoja huo alionekana kuunga mkono utawala huo wa Camara nchini Guinea.


Camara ambae utawala wake uliwakamata wanajeshi 20 kwa kushukiwa kupanga njama za kumpindua,ametagaza hatagombea katika uchaguzi wa wa tarehe tatu 13 mwezi Disemba mwaka huu. Iwapo atabadili msimamo wake huenda hatua hiyo ikaitia hofu jamii ya kimatifa hasa ikizingatiwa kuna tabia ya viongozi nchini Guinea kungagania kubakia madaraka.

Mwandishi Jane Nyingi / RTRE

Mhariri:M.Abdul-Rahman • Tarehe 05.05.2009
 • Mwandishi Jane Nyingi/ AFPE..Picha AFP
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/HkL7
 • Tarehe 05.05.2009
 • Mwandishi Jane Nyingi/ AFPE..Picha AFP
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/HkL7
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com