TEHRAN : Putin aonya dhidi ya kuishambulia Iran | Habari za Ulimwengu | DW | 17.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEHRAN : Putin aonya dhidi ya kuishambulia Iran

Rais Vladimir Putin wa Urusi ameonya dhidi ya kuchukuliwa kwa hatua ya kijeshi kwa Iran na ameunga mkono haki ya nchi hiyo kuwa na nishati ya nuklea.

Putin ameweka wazi hapo jana kwa serikali ya Marekani kwamba Urusi haitokubali kuchukuliwa kwa hatua ya kijeshi dhidi ya Iran na amemwalika Rais Mahmoud Ahmedinejad wa Iran mjini Msocow kwa mazungumzo.

Putin ametowa mwaliko huo kwa Ahmedinejad ambaye ametengwa na mataifa ya magharibi yanayohofia kwamba mpango wa nuklea wa nchi hiyo ni kisingizio cha kutengeneza mabomu ya nuklea baada ya mkutano wa mataifa ya bahari ya Caspian ya Kazakhstan na Turmeknistan ambayo yamefuta uwezekano wa kukubali kushambuliwa kwa Iran kupitia ardhi zao.

Kauli hiyo ya Putin inaonyesha tafauti kati ya mataifa ya magharibi na Ikulu ya Urusi katika kukabiliana na mpango wa nuklea wa Iran.

Akizungumzia hatari ya uwezekano wa shambulio la kijeshi la Marekani dhidi ya Iran waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Ujerumani Joschka Fischer amesema vitakuwa vita vyengine ambavyo vitaanzishwa lakini bila ya ushindi na kwamba usahihdi wote aliouona umempa imani kwamba hakuna hakikisho kwamba kwa shambulio la kiasi fulani unaweza kuteketeza uwezo wa Iran wa kumiliki silaha za nuklea kwa hiyo unaweza kuishia na vita vyengine vipya vya maafa zaidi na Iran yenye uwezo wa silaha za nuklea.

Rais wa Urusi kufuatia mazungumzo yake na Rais Mahmoud Ahmedinejad amethibitisha kwamba ujenzi wa mtambo wa nuklea wa Bushehr nchini Iran unaojengwa kwa msaada wa nchi hiyo utamalizika kama ilivyopangwa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com