TEHRAN: Iran yasisitiza haki ya kuwa na teknlojia ya kinyuklia | Habari za Ulimwengu | DW | 11.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEHRAN: Iran yasisitiza haki ya kuwa na teknlojia ya kinyuklia

Rais Mahmoud Ahmedinejad wa Iran amekariri msimamo wa Tehran kuwa ina haki ya kuzalisha nishati ya kinyuklia.Alitamka hayo katika hotuba aliyotoa mbele ya umma mjini Tehran,kuadhimisha mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979.Vile vile alisema,Iran ipo tayari kujadiliana na nchi za Magharibi kuhusu mradi wake wa nyuklia,lakini haitokubali dai la kusitisha harakati za kurutubisha madini ya uranium.Wakati huo huo mpatanishi mkuu wa Iran kuhusu suala la nyuklia, Ali Larijani amewaambia wajumbe katika mkutano wa usalama wa kimataifa mjini Munich kuwa mradi wa kinyuklia wa Iran ni kwa ajili ya matumizi ya amani tu.Kwa upande mwingine,waziri wa masuala ya nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier ameuambia mkutano huo,jumuiya ya kimataifa lazima izizuie nchi kama Iran,kupata silaha za kinyuklia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com