Tuliyo nayo: Watu 12 wameuawa baada ya dereva mmoja kulivurumisha lori katika umati wa watu mjini Berlin. Rais wa Urusi Vladmir Putin ameyaita mauaji ya balozi wa Urusi nchini Uturuki kuwa ni uchochezi wa kujaribu kuyaharibu mahusiano baina ya nchi hizo mbili na jopo maalum la wapiga kura nchini Marekani lamchagua Donald Trump kuwa rais.