Siku ya mwisho ya waasi wa FNL Palipehutu kurudi Burundi | Matukio ya Kisiasa | DW | 14.05.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Siku ya mwisho ya waasi wa FNL Palipehutu kurudi Burundi

Leo ni siku ya mwisho waliyopewa waasi wa kundi la FNL Palipehutu kurudi nchini Mwao kwa minajili ya kutekeleza makubaliano ya amani.

Hata hivyo viongozi hao bado wapo nchini Tanzania.Viongozi wa eneo hilo la maziwa makuu walitoa muda wa hadi tarehe 15 maafisa hao wa FNL akiwemo kiongozi wao Agaton Gwasa warudi mjini Bujumbura lakini taarifa zinasema haijulikani ni lini Gwasa atarudi nchini Burundi.

Ili kujua ni kwanini bado maafisa hao wa FNL wako nchini TZ Saumu Mwasimba alizungumza na msemaji wake Pastel Habimana na kwanza alikuwa na haya ya kusema.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com