Sherehe za krismasi.
25 Desemba 2008Matangazo
ROME:
Sherehe za kuadhimisha krismasi zimeanza duniani kote.
Baba mtakatifu Benedikt wa 16 ,kama desturi aliongoza sala jana usiku.
Hapo awali alijitokeza dirishani kwenye uwanja wa mtakatifu Petro na kuwasha mshumaa kama ishara ya amani.Katika ujumbe wake baba mtakatifu ametoa mwito juu ya kukomesha chuki na umwagaji damu katika mashariki ya kati.
Na Katika mji wa Bethlehem, kwenye ukingo wa magharibi, mamia ya watu walijipanga foleni ili kusali katika kanisa la uzawa wa Yesu Kristo.
Kwa mujibu wa historia ya dini ya ukristo,Bethlehem ndiyo mji ambako Yesu Kristo alizaliwa.