Sherehe ya maonesho ya Siku ya Kimataifa ya Yoga 2017 | Mada zote | DW | 22.06.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Sherehe ya maonesho ya Siku ya Kimataifa ya Yoga 2017

Kila mwaka, maonesho makubwa ya Yoga hufanywa tarehe 21 mwezi wa Juni katika sehemu mbalimbali ulimwenguni. Hii ni taswira tu ya sehemu ya sherehe hizo za mwaka huu. Hii ikiwa mwaka wa tatu kwa sherehe hizo.

Je Yoga ni nini?

Ni aina ya zoezi la kiafya linalozingatia namna ya kudhibiti upumuaji, kuweka viungo vya mwili katika namna tofautitofauti huku ukitafakari kuhusu jambo. Zoezi hili hufanywa kwa manufaa ya kiafya na kutuliza akili na mwili. Kulingana na historia, zoezi hili lilianza na jamii ya Wahindi. Kadhalika kwa wanaolienzi, inaaminika kuwa ni zoezi linalowaunganisha washiriki na Mungu. Katika miaka mitatu iliyopita, zoezi hili lilianza kusherehekewa kote ulimwenguni na kutengewa Juni 21 kuwa tarehe yake maalum kusherehekewa kimataifa. Hii hapa baadhi ya picha ya jinsi sherehe zilivyokuwa katika sehemu chache za ulimwengu.