1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Scholz aunga mkono mali za Urusi kuinunulia Ukraine silaha

Lilian Mtono
21 Machi 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema anaunga mkono uamuzi wa kutumia mali za Urusi zilizozuiwa kwa ajili ya kuinunulia silaha Ukraine.

https://p.dw.com/p/4dz28
Kansela wa Ujerumani Olaf Scho
Kansela wa Ujerumani Olaf SchoPicha: Dursun Aydemir/AA/picture alliance

Amesema kabla ya mkutano wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels kwamba mapato hayo yanatakiwa kutumika kununua silaha za kuisaidia Ukraine kujilinda huku akionyesha matumaini kwamba viongozi wenzake watakubaliana juu ya suala hilo.

Ikulu ya Kremlin imesema Umoja wa Ulaya utakuwa umekiuka pakubwa sheria ya kimataifa ikiwa utatumia mali hizo za Urusi, ikiwa ni pamoja na athari zake kwenye uchumi wa Ulaya, taswira na sifa yake.

Huku hayo yakiendelea, Hungary na Slovakia zimesema hazitaunga mkono mkakati unaoongozwa na Jamhuri ya Czech wa kuzalisha na kupeleka silaha nchini Ukraine, hatua inayothibitisha mgawanyiko uliopo baina ya mataifa ya Ulaya kuhusu kuipatia silaha Ukraine.