Sarafu ya Euro yajidhihirisha kuwa ngao ya uthabiti. | Matukio ya Kisiasa | DW | 15.01.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Sarafu ya Euro yajidhihirisha kuwa ngao ya uthabiti.

Nchi za umoja wa sarafu ya Euro hivi sasa zina wakaazi wapatao 320, na sarafu hiyo hivi sasa inaonekana duniani kuwa itatumika katika shughuli za ubadilishanaji fedha katika mabenki.


Kujiunga kwa Slovakia katika umoja wa sarafu wa umoja wa Ulaya kuanzia Januari mosi 2009, kumelifanya eneo hilo linalotumia sarafu ya Euro kuwa na watu karibu milioni 329. Ni mataifa 16 hata hivyo yaliyomo katika umoja huo wa sarafu kati ya mataifa 27 wanachama wa umoja wa Ulaya , sarafu ambayo inaonekana duniani kuwa itatumika katika shughuli za ubadilishanaji fedha katika mabenki. Na katikati ya mzozo wa kifedha duniani sarafu ya Euro inajikuta ikipata nguvu.

Nani aliweza kufikiria , kwanza Euro ilikuwa inafamika kuwa inafanya kila kitu kuwa ghali, na sasa sarafu hiyo inajijenga katika wakati huu wa mzozo wa kiuchumi kuwa ngao ya kuleta uthabiti. Bara la Ulaya ambalo kwa kiasi fulani limeweza kujitoa kutoka katika mzozo huo kirahisi , inapaswa kuishukuru sarafu yake ya Euro. Mzozo wa kifedha kama kwa mfano ulioikumba Hangary ama Lavtia, ingeweza pia kuikumba Ujerumani ama hata Ufaransa, iwapo Euro haingekuwapo. Pale ambapo sarafu ya Euro inatumika imeonekana kuwa kama aina ya kinga. Pia Norbet Walter, mkuu wa kitengo cha uchumi katika benki ya Deutsche bank, ametoa maelezo yanayoleta faraja kwa sarafu ya Euro pamoja na benki kuu ya Ulaya.

Sarafu ya Euro imethibitika kuwa ni sarafu ya pili muhimu , baada ya Dollar ya Marekani . Na benki kuu ya umoja wa Ulaya sio tu katika muda wa miaka kumi iliyopita, lakini pia katika miaka miwili iliyopita imejionyesha katika mzozo huu wa kifedha kuwa inauwezo wa kiutendaji. Nafikiri , kuwa imani hii juu ya uwezo wa benki hiyo umepanda sana duniani kote.


Kwa mfano Hangary na Latvia zinaonyesha , ni kwa kiasi gani zile nchi ambazo hazimo katika nchi zinazotumia sarafu imara ya Euro zinavyoweza kudhoofika. Sarafu ya Hungary ya Forint ingekuwa ni sarafu ya kutumika katika mauzo ya sarafu na hisa duniani, ingeweza pia kuitumbukiza nchi hiyo katika kufilisika.

Matatizo makubwa ya kifedha nchini Latvia , ilibidi kupata kichocheo cha Euro nusu bilioni kutoka kwa shirika la fedha la kimataifa IMF. Hakuna shaka basi ndio sababu Euro ilipata ghafla mashabiki wapya.

Nafikiri , zile nchi ambazo zinaelekea kuwa wanachama wa umoja wa Ulaya na wakati huo huo zikiwa na shaka shaka, hatua ya kuharakisha kujiunga na umoja wa sarafu inapaswa kuwa wazi zaidi. Hii si kwa nchi ndogo ndogo tu, kama zile za eneo la Balkan , lakini hata nchi kama Poland. Ni jambo la kawaida , iwapo nchi hizo tatu, ambazo zingekuwa wanachama tangu mwanzo , zikajadiliwa kwanza. Pia nchi za Denmark, Sweden na Uingereza. Hapa wakati wote kunamatatizo, kwamba Denmark na Sweden sio tu kwamba wanahitaji , lakini upo uwezekano.


Binafsi Uingereza , ambako sarafu ya Euro inaogopewa kama shetani , watu mara tu wameanza kuzungumzia kuhusu sarafu hiyo. Si muda mrefu sana, wakati sarafu ya Paund ya Uingereza ilipokaribiana na Euro , mjadala huo ulianza. Lakini kwa wakati huu sarafu ya Euro inaonekana kuwa na nguvu katika mabadilishano na sarafu ya Dollar.
 • Tarehe 15.01.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GZFl
 • Tarehe 15.01.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GZFl
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com