1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMADI:Wanajeshi wa Marekani waanzisha Operesheni karibu na mpaka wa Syria

1 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEVx

Taarifa za hivi punde zinaeleza kwamba vikosi vya kijeshi vya Marekani na Iraq vikiongozwa na helikopta vimefanya mashambulio katika miji ya karibu na mpaka wa Iraq na Syria mapema hii leo.

Polisi kwenye eneo hilo wamesema misafara ya magari ya kijeshi ya Marekani iliingia katika mji wa Qaim na miji mingine ya karibu ikiwa ni pamoja na Karbila na Sedea mapema hii leo kufuatia mashambulio ya helikopta.Duru za hospitali zimesema watu 10 wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa kwenye mapamabano hayo dhidi ya waasi.

Hata hivyo lakini kumetolewa taarifa za kutatanisha kwamba jeshi la Marekani halina taarifa yoyote kuhisiana na operesheni yoyote kwenye eneo hilo.