1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Syria atoa msamaha mpya kwa wafungwa

21 Juni 2011

Rais wa Syria Bashar al-Assad katika jitahada ya kumaliza machafuko ya umwagaji damu nchini humo, leo ametoa amri mpya ya kuwaachilia huru wafungwa waliofanya uhalifu kabla ya Juni 20 mwaka huu.

https://p.dw.com/p/RUx5
+++NUR FÜR ARTIKEL ZU DIESEM THEMA VERWENDEN+++ In this photo released by the Syrian official news agency SANA, Syrian President Bashar Assad speaks at the Parliament, in Damascus, Syria, Wednesday, March 30, 2011. Syria's president has blamed the wave of protests against his authoritarian rule on 'conspirators' - but he failed to offer any concessions to appease the extraordinary wave of dissent. (AP Photo/SANA) EDITORIAL USE
Rais wa Syria, Bashar al-AssadPicha: AP

Hii ni mara ya pili kwa Rais Assad kutoa msamaha kwa wafungwa katika kipindi kisichopindukia mwezi mmoja. Mwishoni mwa mwezi Mei, aliwasamehe wafungwa wote wa kisiasa waliozuiliwa wakati wa machafuko ya nchini humo. Msamaha wa hii leo, umetolewa siku moja baada ya kiongozi huyo kuahidi kufanya mageuzi kadhaa na kuwa na katiba mpya hivi karibuni.

Katika hotuba yake ya tatu kwa taifa, tangu maandamano ya upinzani kuanza nchini Syria katika mwezi wa Machi, Rais Assad amesema, majadiliano ya kitaifa huenda yakafungua njia ya kufanywa mageuzi katika katiba au kuwa na katiba mpya, lakini akaongezea kuwa hakutokuwepo mageuzi yo yote wakati wa machafuko.

Ahadi zake mpya za mageuzi hazikuweza kuwaridhisha wapinzani wake, walioapa kuendelea na maandamano yao. Mwanasheria maarufu wa haki za binadamu, Anwar al-Bunni alieachiliwa huru mwezi uliopita baada ya kuwa jela miaka mitano amesema, hotuba ya Assad inavunja moyo. Akaeleza kuwa madai muhimu ya umma wala hayakutajwa katika hotuba hiyo na kwamba amepuuza ukweli kuwa nchi hiyo inakabiliwa na mzozo wa kisiasa.

Wakati huo huo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Victoria Nuland amesema, kinachohitajiwa hivi sasa ni vitendo na sio maneno: hotuba ni maneno tu. Barani Ulaya, mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuimarisha vikwazo dhidi ya Rais Assad kwa sababu ya umwagaji damu unaosababishwa nchini humo katika kupambana na maandamano ya upinzani. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle amesema :

Bundesaußenminister Guido Westerwelle (FDP) nimmt am Montag (02.05.2011) in Berlin Stellung zum Tod von Terrorchef Osama Bin Laden. US-Spezialeinheiten konnten den Führer der Terrororganiastion Al-Kaida in Pakistan töten. Westerwelle hat die Tötung Osama bin Ladens begrüßt. Bin Laden sei einer der «brutalsten Terroristen der Welt» gewesen, der das Leben von mehreren tausend Menschen auf dem Gewissen habe. Foto: Maurizio Gambarini dpa
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido WesterwellePicha: picture alliance / dpa

"Sisi huku Ulaya tumekubaliana vikwazo zaidi. Kilichobaki ni kupata idhini bayana kutoka Umoja wa Mataifa."

Wakati huo huo,Ufaransa ikizidi kuushinikiza Umoja wa Mataifa, imesema, haiwezekani tena kwa Baraza la Usalama la umoja huo, kuendelea kukaa kimya.

ARCHIV: Frankreichs Premierminister Francois Fillon, aufgenommen waehrend einer Pressekonferenz in Berlin (Foto vom 10.03.10). Fillon hat am Samstag (13.11.10) sein Amt niedergelegt. Staatspraesident Nicolas Sarkozy habe den Ruecktritt akzeptiert, teilte der Elysee-Palast mit. Foto: Michael Kappeler/ddp/dapd
Waziri Mkuu wa Ufaransa, Francois FillonPicha: AP

Waziri Mkuu wa Ufaransa, Francois Fillon, alipozungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari mjini Paris, akiwa na waziri mkuu mwenzake wa Urusi, Vladimir Puitin alisema, wakati umewadia kwa kila mmoja kuwajibika. Lakini, Urusi mara nyingine tena, imesema, kuwa inapinga kuingilia kati mambo ya ndani ya mataifa huru.

Maandamano ya upinzani yanaendelea nchini Syria tangu Machi 15, licha ya serikali kutumia mabavu dhidi ya wapinzani wake. Kwa mujibu wa makundi ya kimataifa ya haki za binadamu, zaidi ya watu 1,300 wameuawa na zaidi ya 10,000 wengine wamekamatwa kiholela. Rais wa Halmashauri ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu, Jakob Kellenberger amesema, ombi la kuwa na uhuru wa kutembelea maeneo yaliyokumbwa na maandamano na machafuko katika miezi ya hivi karibuni, limeungwa mkono na serikali ya Rais Assad.

Mwandishi:MartinPrema/dpae,afpe

Mhariri:Abdul-Rahman