Rais wa Ecuador pamoja na Chavez | Habari za Ulimwengu | DW | 18.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Rais wa Ecuador pamoja na Chavez

RIYADH:

Viongozi wenye siasa kali na wale wastani ndani ya Jumuiya ya nchi zinazosafirisha mafuta ulimwenguni-OPEC wamegawika juu ya mwito war ais Hugo Chavez wa Venezuela kuwa umoja huo utumike pia kama silaha ya kisiasa.

Rais Rafael Correa wa Ecuador,katika hotuba yake ya kwanza hadharani tangu nchi yake kujiunga tena na OPEC amemuungamkono rais Chavez na kusema umoja huu wa nchi 13 unapaswa kuchukua sura zaidi ya kisiasa.Alisema pia bei za mafuta wakati huu ziko chini.

Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia ameukaripia mwito wa rais Chavez.

Viongozi hao wakubaliana lakini kutetea bei ya juu ya mafuta ya poetroli ya hadi dala 100 kwa pipa.

Rais Chavez alitoa pia onyo kwamba bei ya mafuta yaweza hata kupanda na kufikia dala 200 kwa pipa endapo Marekani ikiihujumu Iran,nchi ya pili itoayo mafuta kwa wingi katika Jumuiya ya OPEC. OPEC imejitolea kutoa mchango wake katika kupambana na dhara za uchafuzi wa hali ya hewa.Saudi Arabia imetangaza kuchangia dala milioni 300 katika juhudi hizo.Indonesia imependekeza Opec itumie centi 60 kutoka kila pipa katika mchango wa kulinda mazingira.

TEHERAN:

Rais Hugo Chavez wa Venezuela anatazamiwa kuwasili jioni ya leo mjini Teheran,kutoka Saudi Arabia, hivyo akibainisha tena usuhuba mkubwa kati ya mahasimu hawa 2 wa Marekni.

Rais Chavez ataandamana na mawaziri 5 miongoni mwao waziri wake wa mambo ya nje,m yule wa mafuta na waviwanda.

Msemaji wa wizara ya nje ya Iran Mohammed Ali Hosseini amesema rais huyo wa Venezuela atatia saini mapatano juu ya ushirikiano wa kiviwanda wakati wa ziara yake hiyo ya siku 1.lHii itakua ziara ya 4 ya rais Chave nchini Iran tangu rais Ahmadinejad kushika madaraka 2005.Ziara yake ya mwisho mjini Teheran ilikua July, mwaka huu alipojenga msingi pamoja na rais Ahmadinejad wa kiwanda cha pamoja cha petroli.Ziara ya mwisho ya rais wa Iran nchini venezela, ilikua Septemba.Ilikua ni ya 3.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com