Rais Jonathan anaongoza katika matokeo ya uchaguzi | Matukio ya Kisiasa | DW | 18.04.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Rais Jonathan anaongoza katika matokeo ya uchaguzi

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan anaongoza katika matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwishoni mwa wiki huku akiwa na zaidi ya kura milioni 22 ambazo tayari zimehesabiwa kutoka kwenye majimbo 35 kati ya 36.

default

Rais wa Nigeria aliyeko madarakani, Goodluck Jonathan

Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa matokeo yaliyotolewa jana Jumapili. Tume huru ya uchaguzi ya Nigeria bado inasubiri matokeo kutoka kwenye jimbo moja na maeneo mengine kadhaa.

Idadi kubwa ya karibu watu milioni 73 na nusu waliojiandikisha kupiga kura walijitokeza katika uchaguzi huo wa rais uliofanyika Jumamosi iliyopita.

Muhammadu Buhari Nigeria Wahl

Mpinzani mkuu wa Rais Goodluck Jonathan, Jenerali Muhammadu Buhari

Mpinzani mkuu wa Rais Jonathan, Muhammadu Buhari ambaye ni kiongozi wa zamani wa kijeshi, amepata kiasi kura milioni 11, nyingi zikiwa zimepigwa katika maeneo ya kaskazini ya nchi hiyo.

Katika taarifa ya awali ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi huo kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi-ECOWAS umeuelezea uchaguzi huo katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika kuwa huru, wa haki na kuaminika. Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutangazwa leo.

 • Tarehe 18.04.2011
 • Mwandishi Kabogo, Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/10vEn
 • Tarehe 18.04.2011
 • Mwandishi Kabogo, Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/10vEn

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com