1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Qatar yahimiza kumalizika kwa mgogoro wa Marekani na Israel

21 Aprili 2026

Qatar imeitolea wito Iran na Marekani kumaliza mgogoro wao wakati muda wa mwisho wa wiki mbili za usitishwaji vita baina yao ukikaribia kuisha usiku wa leo.

https://p.dw.com/p/5Cc1C
Katar Doha 2025 |  Majed Al Ansari
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa nchi hiyo Majed al-Ansari Picha: Imad Creidi/REUTERS

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa nchi hiyo  Majed al-Ansari amesema vita hivyo vimeiweka kanda nzima, uchumi wa dunia na masoko ya nishati hatarini.

Al Ansari alijizuwia kuzungumzia kule kulikoitwa kufeli kwa mazungumzo ya Pakistan akisema dunia nzima inaunga mkono juhudi za Islamabad.

Ameongeza kuwa Qatar bado ina matumaini na inapendekeza angalau kurefushwa kwa muda wa usitishwaji mapigano iwapo makubaliano ya haraka hajatopatikana hadi.

"Ikiwa makubaliano hayakufikiwa, Qatar inaunga mkono hali ya sasa ya usitishaji vita, na tunategemea kuona muendelezo wa usitishwaji vita huo, hadi pale patakapopatikana suluhisho la kidiplomasia. Hapatamfaidi yoyote iwapo tutarejea katika uhasama."

Siku ya Jumapili Rais wa Marekani Donald Trump alisema ametuma ujumbe wake Pakistan, kuhudhuria mazungumzo hayo ambayo hadi sasa hayana uhakika wa kufanyika. Iran bado haijatuma wajumbe wake huko.