POSTDAM : Mkutano wajadili mabadiliko ya hali hewa | Habari za Ulimwengu | DW | 15.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

POSTDAM : Mkutano wajadili mabadiliko ya hali hewa

Maafisa wa mazingira wa kundi la mataifa ya kitajiri duniani na mataifa matano yanayoinukia kiuchumi wameanza mkutano wa siku tatu mjini Postdam Ujerumani unaolenga mpango wa Umoja wa Ulaya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Waziri wa mazingira wa Ujerumani Sigmar Gabriel amezitaka nchi zinazoendelea kujihusisha zaidi katika jitihada za kupambana na kuongezeka kwa kiwango cha ujoto duniani.Ujerumani ni mwenyeji wa mazungumzo hayo ikiwa kama rais wa sasa wa Kundi la Mataifa Manane yenye Maendeleo ya Viwanda Duniani.

Mazungumzo hayo ya Postdam pia yatahudhuriwa na Kamisheni ya Umoja wa Ulaya,mashirika ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Kutunza Mazingira Duniani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com