1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Chama cha rais Sarkozy chashinda uchaguzi

18 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqf

Chama cha kihafidhina cha rais Nicolas Sarkozy kimeshinda raundi ya pili ya uchaguzi wa bunge nchini Ufaransa.

Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi huo chama cha Nicolas Sarkozy cha UMP na washirika wake, kilishinda viti 346 kati ya viti 577 bungeni.

Hata hivyo chama hicho hakikupata kura nyingi sana kama ilivyotabiriwa hapo awali.

Chama cha kisoshalisiti pia kilijiimarisha kwa kupata kura nyingi katika uchaguzi huo.

Waziri mkuu wa zamani wa Ufaransa Iain Juppé alishindwa kupata kiti bungeni hivyo atapoteza wadhifa wake kama waziri wa mazingira na kama naibu kiongozi.

Wapigaji kura asilimia 60 walishiriki kwenye zoezi zima la uchaguzi huo.