Nuremberg, Ujerumani. Mafua ya ndege yaingia Ujerumani. | Habari za Ulimwengu | DW | 25.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Nuremberg, Ujerumani. Mafua ya ndege yaingia Ujerumani.

Maafisa nchini Ujerumani wametoa ishara ya tahadhari na kuzuwia watu kufika karibu na maziwa mawili katika jimbo la Bavaria baada ya bata saba waliochunguzwa kukutwa na virusi vya H5N1 vya mafua ya ndege,likiwa ni tukio la kwanza lililoripotiwa nchini Ujerumani mwaka huu.

Maafisa wa mji wa Nuremberg , wameonya watu kutowakaribia bata maji katika maziwa hayo baada ya bata watano kukutwa na virusi hivyo vya mafua ya ndege.

Matokeo ya uchunguzi zaidi yanatarajiwa katika muda wa siku chache zijazo. Mafua ya ndege yameripotiwa mapema mwezi huu katika jamhuri ya Chek na pia virusi hivyo vimejitokeza katika maeneo mengine katika umoja wa Ulaya mwaka huu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com