NEW YORK:Majeshi ya Shirika kuhudumu Darfur kwa mwaka mmoja
17 Julai 2007Matangazo
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon anatowa wito wa kuidhinishwa kwa haraka hatua ya kupeleka majeshi ya kulinda usalama ya Umoja wa Afrika yatakayoshirikiana na yale ya Umoja wa mataifa katika eneo la Darfur nchini Sudan.
Wiki jana Uingereza,Ufaransa na Ghana zilisambaza azimio lililodurusiwa la Baraza la usalama la umOJA WA mataia linaloidhinisha hatua hiyo.Majeshi hayo yanatarjiwa kuanza kazi kwa muda wa mwaka mmoja kwanza.