NEW YORK: Mwito kulaani mashambulizi ya Israel
25 Mei 2007Matangazo
Wanadiplomasia wa Kipalestina wametoa mwito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulaani mashambulizi ya angani yanayofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza na kukamatwa kwa zaidi ya wanachama 33 wa Hamas wa ngazi ya juu.Waziri wa elimu Nasseredine al-Shaer,wabunge § na wameya 4 ni miongoni mwa wanachama waliokamatwa,baada ya Ukingo wa Magharibi kuvamiwa na wanajeshi wa Israel.