1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu kukutana na Trump Desemba 29 kuhusu Gaza

9 Desemba 2025

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu atafanya mazungumzo na Rais wa Marekani Donald Trump mnamo Desemba 29 ili kujadili hatua zinazofuata katika mpango wa amani kuhusu Gaza unaosimamiwa na Marekani.

https://p.dw.com/p/54zKF
Jerusalem | Rais Donald Trump akisalimiana na Benjamin Netanyahu
Rais wa Marekani Donald Trump (kushoto) akisalimiana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu huko Jerusalem: 13.10.2025Picha: Saul Loeb/REUTERS

Netanyahu anatarajiwa kukutana na Trump huko Florida huku serikali ya Marekani ikijaribu pia kumshawishi Rais wa Misri Abdel-Fattah al-Sissi kuhudhuria mazungumzo hayo.

Taarifa hii imetolewa baada ya Netanyahu kusema kuwa awamu ya pili ya kusitisha mapigano katika  Ukanda wa Gaza  itaendelea mara tu Hamas itakapokamilisha zoezi la kurejesha mabaki ya mateka wa mwisho.