NAIROBI : Uchaguzi mkuu Kenya kufanyika Desemba | Habari za Ulimwengu | DW | 13.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAIROBI : Uchaguzi mkuu Kenya kufanyika Desemba

Rais Mwaki Kibaki wa Kenya amesema hapo jana kwamba Kenya itakuwa na uchaguzi wake mkuu wa nne nchini humo hapo mwezi wa Desemba na kwamba hata angelipendelea uchaguzi huo ufanyike mapema zaidi.

Baadhi ya wabunge walipendekeza kucheleweshwa kwa uchaguzi huo ambao unatarajiwa kuwa wa mchuano mkali kuwahi kushuhudiwa katika taifa hilo la watu milioni 36 lenye nguvu kubwa za kiuchumi Afrika Mashariki.

Kibaki amewaambia waandishi wa habari kwenye maonyesho ya kilimo mjini Nakuru kwamba suala la kuahirisha uchaguzi huo halipo kabisa na kwamba uchaguzi huo utafanyika katika kipindi cha mwezi wa Desemba.

Wapinzani wanaishutumu serikali yake kwa kujaribu kuutumia kwa faida yake uchaguzi huo kwa kuwanyima wapiga kura kadi za vitambulisho katika maeneo ya wapinzani pamoja na kuhoji suala la upendeleo kwenye tume ya uchaguzi ambayo wajumbe wake wengi wamechaguliwa na rais huyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com